• HABARI MPYA

    Friday, November 29, 2013

    KOCHA MPYA AZAM AWASILI KESHO DAR, AMEWAHI KUWAFUNDISHA AKINA ETO’O, ALIWAPA WAKONGO KOMBE LA AFRIKA MWAKA JANA

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    KOCHA mpya wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog aliyeipa Leopard FC ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), taji la Kombe la Shirikisho Afrika mwaka jana anatarajiwa kuwasili kesho nchini kusaini Mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
    Mchezaji huyo wa zamani wa Yaounde ni mwalimu wa kiwango cha juu cha ufundishaji soka na elimu ya viungo aliyehitimu vizuri mafunzo yake katika Chuo cha Vijana na Michezo, INJS mjini Yaounde. Alikwenda kujiendeleza kielimu nchini Ujerumani na kwa pamoja na Pierre Njili na Martin Ndtoungou walipata Stashahada za ukocha na leseni za UEFA daraja la B mwaka 1987. 
    Joseph Marius Omog, kocha mpya wa Azam FC

    Aliporejea nchini mwake, Joseph Marius Omog, alifundisha timu kadhaa kama Fovu ya Baham na Aigle ya Menoua na akazifikisha fainali ya Kombe la Cameroon klabu zote. 
    Mwaka 2001 aliteuliwa kuwa Msaidizi wa kocha Mjerumani, Winfried Schafer katika timu ya taifa ya Cameroon, Simba Wasiofungika chini ya Nahodha Samuel Eto’o haswa kutokana na kujua kwake Kijerumani, kwa sababu kocha huyo alikuwa hazungumzi Kiingereza wala Kifaransa. 
    Mwaka 2003 aliteuliwa kuwa kocha Mkuu wa timu ya taifa baada kuondoka kwa Winfried Schafer, lakini akafukuzwa mwaka 2010 kutokana na matokeo mabaya na kushindwa kuiwezesha Cameroon kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.
    Akaamua kutoka nje ya nchi na mwaka 2011 alijiunga na AC Leopard ya Kongo Brazzaville na kuiwezesha kutwaa Kombe mwaka huo huo na kuipa tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho. 
    Na akafanikiwa kuiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe hilo la Afrika kwa kuifunga Djoliba ya Mali mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano na kutengeneza ushindi wa jumla wa 4-3.
    Kwa kifupi huyu ndiye mwalimu mpya wa Azam FC, anayekuja kurithi mikoba ya Stewart Hall, Muingereza aliyeachia ngazi mwezi uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA MPYA AZAM AWASILI KESHO DAR, AMEWAHI KUWAFUNDISHA AKINA ETO’O, ALIWAPA WAKONGO KOMBE LA AFRIKA MWAKA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top