• HABARI MPYA

    Thursday, November 21, 2013

    SERIKALI YA KENYA YATOA DOLA 125,000 CECAFA CHALLENGE, HAKI YA MATANGAZO YA TELEVISHENI YAUZWA KWA DOLA 600,000

    Na Brian Moseti, Nairobi
    SERIKALI ya Kenya imetoa dola za Kimarekani 125,000 (zaidi ya Sh. Milioni 140) kudhamini michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayoanza wiki ijayo mjini Nairobi.
    Hili ni ongezeko la dola za Kimarekani 600,000 (zaidi ya Sh. Milioni 900) zinazotokana na mauzo ya haki za matangazo ya Televisheni yatakayohusu mechi zote 27 za mashindano hayo.
    Watatetea taji? Uganda ndio mabingwa watetezi, walitwaa Kombe hilo mwaka jana nyumbani

    Gavana wa Machakos, Alfred Mutua naye ametoa Sh. Milioni 5 za Kenya zaidi ya Sh. Milioni 11 za Tanzania kudhamini mashindano hayo, wakati wenzake kutoka Nairobi na Kisumu wametoa Sh Milioni 10 za Kenya, zaidi ya Sh. Milioni 22 za Tanzania.
    Kampuni ya Coca Cola pia imetoa Sh Milioni 6.5 za Kenya (Milioni 5 taslimu na vinywaji vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5), wakati kampuni ya Bima ya UAP itatoa Sh Milioni 5.5 za Kenya (Milioni 2.5 fedha taslimu nan a Milioni 3 kwa ajili ya bima za wachezaji na marefa wote) katika mashindano hayo.
    Kama ilivyothibitishwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya, Sam Nyamweya, Serikali ya Kenya pia inakusanya fedha zaidi za kuongeza kwenye mashindano hayo na hivi karibuni itawasilisha mchango wake.
    Michuano hiyo itafanyika katika miji mitano, Nairobi, Kisumu, Mombasa na Machakos kati ya Novemba 27 na Desemba 12, mwaka huu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YA KENYA YATOA DOLA 125,000 CECAFA CHALLENGE, HAKI YA MATANGAZO YA TELEVISHENI YAUZWA KWA DOLA 600,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top