• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 23, 2013

  SIMBA SC YAKALISHWA NA RUVU, ASHANTI YAUA 6-0, MTOTO WA KABUNDA NI NOMA

  Na Mahmoud Zubeiry, Ilala
  SIMBA SC imepoteza mechi ya kwanza katika mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 za klabu za Ligi Kuu Bara, maarufu kama Kombe la Uhai, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
  Issa Abdallah alitangulia kuifungia Simba SC dakika ya kwanza tu, lakini Hamisi Kisuke akaisawazishia Ruvu dakika ya 41 kabla ya Raheem Madega kuifungia bao la ushindi timu hiyo ya Pwani dakika ya 90.
  Mshambuliaji wa Ruvu Shooting Raheem Madega akiwatoka mabeki wa Simba SC leo Uwanja wa Karume. Ruvu ilishinda 2-1.

  Huo ni mchezo wa kwanza Simba SC kupoteza katika mechi tatu, baada ya awali kuzifunga JKT Oljoro 3-0 na Mgambo JKT 5-0, wakati Ruvu nayo inashinda mechi ya kwanza leo.
  Hatima ya Simba SC kuingia Robo Fainali sasa ipo mikononi mwa Ashanti ambayo watacheza nayo kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jioni.
  Katika mchezo mwingine wa leo, Uwanja wa Azam Complex Ashanti imeifunga Mgambo JKT ya Tanga 6-0. 
  Mtoto wa beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga, Salum Kabunda ‘Ninja Msudan’ (marehemu), aitwaye Ally Salum Kabunda amefunga mabao matano peke yake, wakati lingine lililokuwa la kwanza limefungwa na Hussein Mkongo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAKALISHWA NA RUVU, ASHANTI YAUA 6-0, MTOTO WA KABUNDA NI NOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top