• HABARI MPYA

    Tuesday, November 26, 2013

    WACHEZAJI WOTE CHALLENGE WAPEWA BIMA

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    KAMPUNI ya Bima ya UAP leo imetangaza rasmi udhamini wa Sh Milioni 5.5 za Kenya kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayoanza kesho mjini Nairobi, Kenya.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo katika hoteli ya Hillpack mjini hapa, Rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya amesema kwamba udhamini huo unajumuisha fedha taslimu Sh. Milioni 2.5 za Kenya na Milioni 3 kwa ajili ya gharama za bima za wachezaji na marefa wote katika mashindano hayo.
    Mkurugenzi Mkuu wa UAP, James Wambugu kushoto akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 5 za Kenya kwa viongzi wa FKF na CECAFA leo 

    Nyamweya pia amesema kwamba, Serikali ya Kenya imetoa dola za Kimarekani 125,000 (zaidi ya Sh. Milioni 140) kudhamini michuano hiyo, hilo likiwa ni ongezeko la dola za Kimarekani 600,000 (zaidi ya Sh. Milioni 900) zinazotokana na mauzo ya haki za matangazo ya Televisheni yatakayohusu mechi zote 27 za mashindano hayo.
    Amesema pia Gavana wa Machakos, Alfred Mutua naye ametoa Sh. Milioni 5 za Kenya zaidi ya Sh. Milioni 11 za Tanzania kudhamini mashindano hayo, wakati wenzake kutoka Nairobi na Kisumu wametoa Sh Milioni 10 za Kenya, zaidi ya Sh. Milioni 22 za Tanzania.
    Kampuni ya Coca Cola pia imetoa Sh Milioni 6.5 za Kenya (Milioni 5 taslimu na vinywaji vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5), wakati kampuni ya Bima ya UAP itatoa Sh Milioni 5.5 za Kenya (Milioni 2.5 fedha taslimu nan a Milioni 3 kwa ajili ya bima za wachezaji na marefa wote) katika mashindano hayo. Nyamweya amesema pia bado wanatarajia fedha zaidi kutoka serikalini.
    Wansaini Mkataba

    Sam Nyamweya kushoto anagonga muhuri


    Makabidhiano ya Mkataba

    Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa UAP, James Wambugu amesema kwamba kampuni yake imekuwa pia ikiidhamini timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars mbali na ufadhili huu wa CECAFA na amewahakikishia wachezaji na marefa wote wapo salama katika mashindano haya chini ya Bima ya kampuni yake.
    Michuano ya CECAFA Challenge inaanza kesho mjini hapa na Zanzibar itafungua dimba na Sudan Kusini saa 8:00 mchana kabla ya wenyeji, Kenya kucheza na Ethiopia saa mbili baadaye, Uwanja wa Nyayo.
    Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itacheza na Zambia saa 10:00 jioni ya keshokutwa baada ya mechi kati ya Burundi na Somalia itakayoanza saa 8:00 mchana Uwanja wa Machakosi.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI WOTE CHALLENGE WAPEWA BIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top