• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 28, 2013

  DOMAYO: ZAMBIA WATATUTAMBUA

  Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
  KIUNGO wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars amesema anafahamu Zambia ni timu iliyo juu yao kisoka, lakini wanataka kubadilisha picha hiyo leo watakapomenyana na timu hiyo katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.
  Kili Stars inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania taji la nne la Kombe la Challenge leo kwa kumenyana na Zambia Uwanja wa Machakos katika mchezo wa Kundi B utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Somalia na Burundi na Domayo amesema wanataka ushindi.
  Watatutambua; Frank Domayo amesema wanataka kuwafunga Zambia leo

  “Zambia ni timu nzuri kweli, ipo juu yetu katika renki za FIFA, wao wanashiriki mashindano mengi makubwa, lakini pamoja na yote tunataka kuwafunga na tutawafunga,”alisema.
  Domayo amesema kinachompa ujeuri wa kusema hivyo ni ubora wa kikosi cha Stars kwa sasa na dhamira ambayo wachezaji wengi wanayo kwa sasa, kurejesha heshima.
  “Unajua katikati hapa tumewaudhi wapenzi baada ya timu kufanya vibaya, ila kupitia mashindo haya tunataka turejeshe heshima yetu, na tutapambana,”alisema.         
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DOMAYO: ZAMBIA WATATUTAMBUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top