• HABARI MPYA

    Sunday, November 24, 2013

    RAGE AMTEUA MICHAEL WAMBURA KAMATI YA UTENDAJI SIMBA, AGOMA KUITISHA MKUTANO MKUU KWA AMRI YA TFF

    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
    MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage ameligomea Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na kusema kuwa haitishi mkutano wa dharura alioagizwa na akilazimishwa atajiuzulu na pia amemteua Michael Wambura kuwa Mjumbe mpya wa Kamati ya Utendaji ya klabu.
    Rage aliyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo.
    Rage ambaye ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), alisema kuwa kwa mujibu wa katiba ya Simba ibara ya 28/a,b, c, d, muundo wa kamati ya Utendaji inasema Simba haina Kaimu makamu mwenyekiti.

    “Kwa mujibu wa katiba ya Simba, sisi hatuna Kaimu Makamu Mwenyekiti bali tuna Makamu Mwenyekiti ambaye alijiuzulu na alikuwa na kazi mbili tu kwa mujibu wa katiba moja ni kufanya yale aliyoelekezwa na Mwenyekiti, na kufanya kazi wakati mwenyekiti hayupo hivyo mwenye mamlaka ni mimi,”alisema.
    Alisema kuwa kwa mujibu wa katiba anatakiwa aitishe vikao mara 4 kwa mwaka ila yeye amefanya vikao 12 mpaka sasa.
    Rage aliyekifananisha kikao cha kikao cha harusi alimshukuru Jamal Malinzi kwa kumtambua kuwa badio Mwenyekiti wa Simba.
    Alisema kuwa ameliandikia barua TFF, na kuwajulisha kuwa kamati yake imevunja katiba ya Simba, TFF, CAF, na Fifa, na ana ushahidi na hilo.
    “Nina ushahidi wa CD za sura za watu na maneno sambamba na Docoment iliyosajiliwa na Kaimu Mwenyekiti Joseph Itang’are, na katiba ya TFF inasema atakayevunja basi adhabu yake 
    ni kufungiwa kwa miaka 10 kujihusisha na soka,”alisema
    Rage aliendelea kusema kuwa amepata maagizo ya TFF ya kuitisha mkutano wa dharura ambapo wametumia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema: “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”
    Alisema kuwa anakubali wao ni wanachama wa TFF ila kwanini wamnyanganye madaraka na kumpangia agenda za kikao na kumpa mda wa kufanya mkutano huo.
    “Siitishi mkutano wa dharura nalinda katiba yangu ya Simba na TFF kwani hakuna kipengele hata kimoja kinachosema kuwa nipangie ajenda na kuninyanganya madaraka yangu,”alisema.
    Alisema kuwa kwa mujibu wa katiba ya Simba ibara ya 22 mwenye mamlaka ya kuitisha mkutano ni mwenyekiti wa klabu na kama ataona inafaa kufanya hivyo.
    “Tuheshimu Katiba jamani, sio kumpangia mtu cha kufanya na agenda ya kujadili siku hiyo,”alisema.
    Alisema alitegemea suala hilo lao la  mgogoro lingepelekwa TFF wangelipeleka kwenye kamati ya sheria na maadili, sio kamati ya utendaji kama walivyofanywa.
    “Katiba ya TFF haina mamlaka ya kujadili mambo ya kisheria, nilitegemea suala hili lingepelekwa kwenye kamati husika sio kamati ya utendaji,”alisema.
    Wakati akiendelea na msimamo huo, Suala la Mshambuliaji Emanuel Okwi hakuliacha nyuma na kusema kuwa sakata hilo alishalimaliza kwenye mkutano wa wanachama wa 2012.
    “Sisi ni watu wazima suala hili lilijadiliwa kwenye mkutano mkuu kwanini linatajwa tena mwaka huu wakati majibu yake watu wote wanayo,”alisema.
    Alisema kuwa mpaka sasa anadaiwa Dola 40 alizokopa Desemba 9 tulipoingia mkataba wa miaka miwili na winga huyo ila walikubaliana akipata timu basi atolewe. “Suala la Okwi kila mtu anajua na tumewasilisha malalamiko yetu FIFA baada ya ile timu ya Etode Saleh ya Tunisia kudai kukubwa na janga la uchumi na kutuomba tuwape hadi Septemba 30 hivyo bado tunasubiri,”alisema
    Akijibu tuhuma za haki za televisheni, Rage alisema kuwa suala hilo ni la Shirikisho za Soka Tanzania (TFF) na kuhoji kwanini wajumbe ya kamati ya utendaji zilipotolea milioni 100 hawakugoma.
    “Mbona zilipotoka zile hela hakuna aliyesema hazitaki, na kufanya tutangaze dhahiri bila siri yoyote ile,”alisema
    Alisema kuwa anawashangaa waliomgeuka na kwenda kwenye mkutano wa mazungumzo na kampuni ya Zuku huko Nairobi ambapo waliwakiliswa na mzee Kinesi na Aveva
    “Oh kulikuwa na makubaliano ya Zuku, wakati mimi mwenyekiti sikupewa taarifa, ila kama wakisema wanaleta million 7000 za udhamini wa haki ya televisheni najiuzulu kesho,”alisema.
    Mbunge huyo aliyemwaga machozi hadharani wakati akiendelea kufunguka alisema kuwa amechoshwa na vitimbi,  nimedhalilishwa vya kutosha nimechoka,”alisema.
    Wakati huo huo Rage alitangaza kumteuwa Michael Wambura kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, baada ya Malkia wa Nyuki kuomba kuondolewa kwenye kamati hiyo kwakuwa na mambo mengi.
    “Tumemuomba Malkia wa Nyuki awe mdhamini wetu hivyo tutapeleka jina lake kwenye mkutano mkuu,”alisema.
    Alisisitiza kuwa mkutano wa Desemba moja ameufuta na ule alioagizwa na TFF kwani yeye ndio mwenyekiti na akilazimishwa kufanywa hivyo atajiuzulu.
    “Heshima yangu mimi ni mbunge wa Taifa linaelewa hivyo, wanasahau nilikuta pazia za magunia klabuni na  umeme hawana kwa miaka 18 zaidi, huku milango wakikodisha sh 200,000 lakini sasa milango ya fremu ni milioni 2 wananiona mbaya,”alisema.
    Alisema kuwa Simba walifaidika na nini kwenye fedha za kuuzwa Henry Joseph, Haruna Moshi Boban, Seleman Matola na kumng’angania kwenye wachezaji wawili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAGE AMTEUA MICHAEL WAMBURA KAMATI YA UTENDAJI SIMBA, AGOMA KUITISHA MKUTANO MKUU KWA AMRI YA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top