• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 28, 2013

  CHUJI APAGAWA NA MAKINDA STARS, ASEMA WADOGO WA UMRI MAMBO MAKUBWA

  Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
  KIUNGO mkongwe wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Athumani Iddi ‘Chuji’ au Kaka Mkuu, amesema kwamba wachezaji chipukizi waliomo kwenye kikosi hicho ni wazuri sana na anaamini watakuwa tegemeo la taifa muda si mrefu.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Chuji alisema kwamba amekuwa akiona vitu ambavyo wanafanya makinda hao mazoezini na anakubali wanajua.
  Kaka Mkuu; Athumani Iddi 'Chuji' amesema wachezaji chipukizi Stars ni wazuri

  “Watoto wanajua sana, hadi raha. Hata kucheza nao unafurahi yaani. Mimi nakuambia hii timu ni bora sana iliyokuja huku (CECAFA Challenge), na nina matumaini tutafanya vizuri,”alisema kiungo huyo wa Yanga SC.
  Chipukizi waliojumuishwa kikosi cha Stars ni Himid Mao, Michael Pius, Ismail Gambo ‘Kussi’, Hassan Dilunga, Elias Maguri, Joseph Kimwaga, Farid Mussa, Juma Luizio, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Haroun Chanongo.  
  Kili Stars inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania taji la nne la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo kwa kumenyana na Zambia Uwanja wa Machakos katika mchezo wa Kundi B utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Somalia na Burundi.         
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHUJI APAGAWA NA MAKINDA STARS, ASEMA WADOGO WA UMRI MAMBO MAKUBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top