• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 28, 2013

  YONDAN: ROBO FAINALI KAMA ‘KUMSUKUMA MLEVI’

  Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
  NAHODHA wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kevin Yondan amesema kwamba wana uwezo wa kuingia Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge tena bila kupoteza hata mchezo mmoja.
  Akizungumza jana mjini hapa, Yondan amesema kwamba kocha Kim Poulsen ameteua kikosi bora sana ambacho kinaweza kufanya kile ambacho wengi miongoni mwa Watanzania hawatarajii kwa sasa.
  Sura ya Nahodha; Kevin Yondan amesema Robo Fainali nyepesi tu kwao. Chini ni beki pacha wake, Said Morad

  “Tuna timu nzuri, nimeona mazoezi yetu kwa kweli yanakwenda vizuri. Mfano pale nyuma mimi ni Morad (Said) wote mabeki wazuri na tutaunda ukuta mzuri, viungo na washambuliaji wote safi  kwa kweli tuko vizuri,”alisema.
  Yondan alisema timu yao itaongezeka makali washambuliaji wawili wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu watakapowasili.
  Wachezaji hao wanasubiri kuichezea klabu yao, Mazembe Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sfaxien ya Tunisia Novemba 30 mjini Lubumbashi na Desemba 1 watawasili mjini hapa. 
  Kili Stars inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania taji la nne la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo kwa kumenyana na Zambia Uwanja wa Machakos katika mchezo wa Kundi B utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Somalia na Burundi.         
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YONDAN: ROBO FAINALI KAMA ‘KUMSUKUMA MLEVI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top