• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 29, 2013

  MAGURI ASEMA ZAMBIA ‘WAMEMTOA UBARIDI’ SASA KENYA ITAMJUA YEYE NANI

  Na Mahmoud Zubeiry Nairobi
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Elias Maguri amesema kwamba mchezo wa jana wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki  Kati, CECAFA Challenge dhidi ya Zambia umemjenga sana na sasa anatarajia kufanya vizuri.
  Akizungumza baada ya mechi ya jana, Maguri anayechezea klabu ya Ruvu Shooting ya Pwani, amesema kwamba mabeki wa Zambia walimpa misukosuko lakini hakurudi nyuma anakaendelea kuwasumbua.
  Elias Maguri jana aliitia misukosuko ngome ya Zambia

  “Wakati natoka, mmoja wao alinifuata akasema mimi ni mdogo lakini ni hatari, akasema niongeze juhudi nitacheza Ulaya, nilifarijika sana,”alisema Maguri akizungumza na BIN ZUBEIRY jana baada ya mechi.
  Elias Maguri alicheza kwa dakika 72 jana kabla ya kumpisha Haroun Chanongo kumalizia mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Kenyatta, Machakos.
  Kwa ujumla Maguri kama ilivyo chipukizi mwenzake kwenye timu hiyo, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar hawa ni tegemeo la baadaye la taifa katika safu ya ushambuliaji.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAGURI ASEMA ZAMBIA ‘WAMEMTOA UBARIDI’ SASA KENYA ITAMJUA YEYE NANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top