• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 29, 2013

  TFF YAMKAMATA PAZURI RAGE, ATAKE ASITAKE SASA ATAITISHA MKUTANO SIMBA SC

  Na Princess Asia, Dar es Salaam
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), sasa limekamata pazuri Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage anayekwepa kuitisha Mkutano Mkuu wa klabu yake, kutokana na agizo lake la kuwataka wanachama wake kufanyia marekebisho katika katiba zao kwa kuingiza ibara ya Kamati za Maadili.
  Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Rage sasa amenaswa na TFF juu ya kuitisha Mkutano

  Taarira ya Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura leo imesema kwamba maagizo hayo yanatokana na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF iliyoketi Novemba 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jamal Malinzi ambapo pamoja na mambo mengine ilijadili umuhimu wa wanachama wake kuunda kamati hizo.
  “Wanachama wa TFF ambao muda wao wa uchaguzi umekaribia, wanatakiwa kufanya marekebisho hayo kwanza kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi. TFF ina aina tatu za wanachama. Wanachama hao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na Klabu za ligi Kuu,”amesema Wambura.
  Rage yupo katika wakati mgumu Simba SC, baada ya kusimamishwa na Wajumbe wake wa Kamati ya Utendaji kwa tuhuma za kuongoza klabu kama mali yake binafsi, bila kushirikisha wenzake.
  Hata hivyo, TFF haikuyatambua mapinduzi hayo na ikamuagiza Rage aitishe Mkutano ndani ya siku 14. Rage naye alisema hawezi kuitisha Mkutano huo, kwa sababu atakuwa anakiuka Katiba ya Simba SC, lakini sasa atalazimika kuitisha Mkutano wa kupitisha marekebisho ya Katiba kwa agizo la TFF. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAMKAMATA PAZURI RAGE, ATAKE ASITAKE SASA ATAITISHA MKUTANO SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top