• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 24, 2013

  SIMBA NA YANGA ZOTE ZACHAPWA UHAI LAKINI ZATINGA ROBO FAINALI, MTOTO WA KABUNDA AENDELEZA MOTO WAKE

  Na Mahmoud Zubeiry, Ilala
  WATANI wa jadi, Simba na Yanga wote wamefungwa sawa, mabao 2-1 kila mmoja jioni ya leo katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya timu za Ligi Kuu ya Bara, maarufu Kombe la Uhai, lakini bahati nzuri kwao, wote wamesonga Robo Fainali.
  Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, Yanga ilichapwa mabao 2-1 na JKT Ruvu ambayo hata hivyo imetolewa.
  Wachezaji wa JKT Ruvu wakishangilia ushindi dhidi ya Yanga leo 
  Yanga ilitangulia kupata bao dakika ya 31 mfungaji Hamisi Issa, lakini JKT ikasawazisha kupitia kwa Mwinyi Hamisi dakika ya 61 na Anwar Kilemile akafunga la pili dakika ya 67.

  Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Ashanti United imeichapa Simba SC mabao 2-1. Simba pia ilitangulia kupata bao dakika ya 11 kupitia kwa Mohamed Salum kabla ya Ally Salum Kabunda kuisawazishia Ashanti dakika ya 18 na Hussein Mkongo akafunga la pili dakika ya 43.   
  Ashanti, Simba na Yanga zote zimeingia Robo Fainali zikiungana na Coastal Union, Mtibwa Sugar, Azam FC, Prisons na JKT Oljoro.
  Robo Fainali za kwanza zitachezwa Novemba 26, Coastal na Oljoro, Prisons na Azam na za pili zitachezwa Novemba 27, Ashanti na Yanga na Mtibwa na Simba SC, zote Uwanja wa Azam Complex. Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZOTE ZACHAPWA UHAI LAKINI ZATINGA ROBO FAINALI, MTOTO WA KABUNDA AENDELEZA MOTO WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top