• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 26, 2013

  YANGA SC WAONYESHWA BONGE LA STRAIKA LA KUWAFUGIA MABAO AFRIKA

  Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
  YANGA SC wanasaka mshambuliaji wa kigeni mkali kwa ajili ya kumtumia katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani na kocha wa Kenya, Harambee Stars, Adel Amrouche amewaonyesha njia.
  Mwalimu huyo amesema atamtegemea mshambuliaji Jacob Keli kumfungia mabao katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge, michuano inayoanza kesho mjini hapa.
  Mchezaji huyo wa KCB, ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya na pia alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu nchini hapa.
  Mchezaji bora; Jacob Keli ni mfungaji bora na mchezaji bora wa Kenya ambaye sasa amepewa jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji ya Harambee Stars katika Challenge

  Hadi sasa bado hajabahatika kuanza katika kikosi cha Harambee, lakini sasa wakati wake umewadia na Amrouche amesema kwamba atamtumia kama mshambuliaji mkuu kwenye mashindano haya.
  “Keli ni mchezaji muhimu katika timu ameonyesha katika msimu huu. Hajapewa nafasi muhimu katika safu ya ufungaji, lakini pia kama kiongozi wa timu. Tutamtegemea yeye kuisaidia timu kwenye mashindano. Jukumu lake litakuwa kama mmoja wa viongozi. Natumaini kwamba atacheza vizuri, kwa sababu amekuwa akifanya hivyo, tutafika mbali kama timu,”alisema.
  Allan Wanga na Keli watatarajiwa kuwa tegemeo la mabao la Kenya na kocha huyo anafikiri wanaweza kucheza kwa ushirikiano mkubwa.
  Harambee Stars inakata utepe wa mashindano kesho kwa kumenyana na Ethiopia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WAONYESHWA BONGE LA STRAIKA LA KUWAFUGIA MABAO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top