• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 29, 2013

  SURE BOY AWA MCHEZAJI BORA CHALLENGE

  Na Mahmoud Zubeiry Nairobi
  KIUNGO wa Tanzania Bara Kilimanjaro Stars, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ jana alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi kati ya timu hiyo na Zambia Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos, Kenya.
  Katika mchezo huo wa Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Bara na Zambia zilitoka sare ya 1-1 na Sure Boy kwa kuwa Mchezaji Bora atazawadiwa kifurushi kutoka Serikali ya Kenya na king’amuzi kutoka DSTV.
  Mchezaji bora; Salum Abubakar 'Sure Boy' jana alikuwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Zambia

  Akizungumza baada ya mchezo huo, kiungo huyo wa Azam FC alisema kwamba mvua iliyonyesha kipindi cha kwanza ilimfanya ashindwe kucheza vizuri mwanzoni, lakini hali ilipobadilika kipindi cha pili akaonyesha uwezo wake.
  “Kwa kweli mvua ilituathiri sana kipindi cha kwanza tukashindwa kucheza, ilituharibia mipango yetu ya michezo kabisa,”alisema mtoto huyo wa winga wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’. 
  Pamoja na hayo, Sure amesema anashukuru japo wamepambana kipindi cha pili na kusawazisha bao hadi kupata sare na kwamba mechi zijazo watajitahidi kushinda dhidi ya Burundi na Somalia.
  Baada ya mechi za jana za Kundi B, Burundi inapanda kileleni kutokana na ushindi wake wa 2-0 dhidi ya Somalia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SURE BOY AWA MCHEZAJI BORA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top