• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 29, 2013

  SUBIRINI MABAO ZAIDI KWA STAILI ILE ILE, ASEMA MKOMBOZI WA STARS JANA MWEDA

  Na Mahmoud Zubeiry Nairobi
  BEKI wa Azam FC Said Morad ‘Mweda’ amesema kwamba baada ya kuifungia Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars bao la kusawazisha dhidi ya Zambia jana, sasa atajitahidi kufunga zaidi kwa staili ile ile ya jana.
  Morad aliifungia Stars bao la kusawazisha dakika ya 48 akiunganisha nyavuni kwa kichwa kona ya kiungio Salum Abubakar ‘Sure Boy’ pia wa Azam FC. 
  Mkombozi wetu; Said Morad jana baada ya kufunga

  “Kwa kweli nimefurahi sana kufunga ambalo limekuwa muhimu leo kwa timu yangu, najua nimewafurahisha Watanzania wenzangu na ninawaahidi furaha zaidi.
  “Mimi kama beki jukumu lango la kwanza ni ulinzi, ila zikitokea nafasi kama hizi za kona nitakuwa napanda kujaribu kurudia mambo kama haya, au unasemaje ndugu yangu,”alisema Morad akiangua kicheko cha tani yake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUBIRINI MABAO ZAIDI KWA STAILI ILE ILE, ASEMA MKOMBOZI WA STARS JANA MWEDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top