• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 30, 2013

  STARS KATIKA MAZOEZI LEO NAIROBI KUJIANDAA NA MCHEZO WA PILI CHALLENGE KESHO

  Kipa wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Ivo Mapunda akizuia mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo leo asubuhi Uwanja wa Chuo Kikuu cha Strathmore, Nairobi, Kenya. Stars inajiandaa kwa mchezo wa pili wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge dhidi ya Somalia Uwanja wa Nyayo, Nairobi kesho mchana.

  Hapa kocha Kim Poulsen anawaelekeza vijana namna ya kukokota mpira

  Anawaelekeza viungo namna ya kuwachzesha washambuliaji

  Anawaelekeza viungo namna ya kukaba wapinzani wanapokuwa na mpira

  Anawaelekeza mabeki namna ya kujipanga wakati kona au mipira ya kutokea pembeni inaelekezwa langoni kwao 

  Anamuelekeza Ivo Mapunda namna ya kujipanga wakati wa kona

  Anawaelekeza mabeki namna ya kujipanga wakati wa kona

  Kipa Aishi Manula akizuia mpira

  Kutoka kulia Kevin Yondan, Salum Abubakar 'Sure Boy' na Said Morad wakifurahia baada ya mazoezi

  Munza vifaa wa timu, Freddy akikusanya mipira baada ya mazoezi

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS KATIKA MAZOEZI LEO NAIROBI KUJIANDAA NA MCHEZO WA PILI CHALLENGE KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top