• HABARI MPYA

    Tuesday, November 26, 2013

    YAYA TOURE AITISHIA AMANI CHELSEA, AWAAMBIA REKODI YAO IKO HATARINI

    KIUNGO Yaya Toure anaamini Manchester City inaweza kuvunja rekodi ya mabao ya msimu katika Ligi Kuu England msimu huu.
    Kiungo huyo wa nguvu amempa jeuri kocha Manuel Pellegrini juu ya uwezo wa kushambulia unaoleta matumaini ya taji kwa kusema rekodi ya Chelsea iko hatarini.
    Kocha Carlo Ancelotti akiwa na kikosi mariadi msimu huu 2009-10 aliiwezesha Chelsea kufunga mabao 103 na kutwaa taji misimu minne iliyopita.
    Jitu la nguvu: Yaya Toure (kushoto, akipambana na Paulinho wa Spurs, amesema City inaweza kuvunja rekodi ya mabao
    Six of the best: Sergio Aguero netted twice in City's rout of Tottenham on Sunday
    Mabao sita: Sergio Aguero alifunga mabao mawili City ikiifumua Tottenham Jumapili
    Put your hands up: Chelsea netted an incredible 103 goals on their way to winning the Premier League in 2010
    Inua mikono juu: Chelsea ilifunga mabao 103 wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 2010

    Na baada ya timu ya Pellegrini kufikisha mabao 34 wakiifunga sita Spurs Jumapili, Toure amesema lengo ni kuvunja rekodi hiyo.
    Alipoulizwa kwamba inaezekana kuipiku rekodi ya Chelsea, alijibu: "Natumaini hivyo — tuna washambuliaji. Watu wawili mbele (Alvaro Negredo na Sergio Aguero) hawa watu huwezi kuamini. Wanajiamini sana.
    "Lakini si kwa sababu ya wachezaji hao wawili tu. Ni timu nzima. Tunashambulia sana na washambuliaji wote wanafurahia hii. Hata (Edin) Dzeko na (Stevan) Jovetic.
    "Timu inaelekeza nguvu zake katika kushambulia. Ni babu kubwa. Na unaposhinda kama tulivyofanya kwa Tottenham ni nzuri. Ni washindani wa kweli katika mbio za taji la Ligi Kuu mwaka huu,".
    Out of action: But even Edin Dzeko is enjoying life at goalscoring City at the moment, claims Toure
    Nje ya Uwanja: Lakini hata Edin Dzeko anafurahia maisha namna ambavyo City inafunga mabao, amesema Toure
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE AITISHIA AMANI CHELSEA, AWAAMBIA REKODI YAO IKO HATARINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top