• HABARI MPYA

  Tuesday, March 06, 2018

  MAN UNITED YATOKA NYUMA KWA 2-0 NA KUIBAMIZA CRYSTAL PALACE 3-2 'KIAJABU AJABU'

  Nemanja Matic akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Manchester United dakika ya mwisho ikitoka nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace na kushinda 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatatu Uwanja wa Selhurst Park, London.
  Andros Townsend alianza kuifungia Palace dakika ya 11 baada ya shuti lake kumbabatiza Victor Lindelof na kumpoteza mwelekeo kipa David de Gea, kabla ya Patrick van Aanholt kufunga kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 48.
  Manchester United ikazinduka, Chris Smalling akifunga la kwanza dakika ya 55, Romelu Lukaku la pili dakika ya 76 na Nemanja Matic la tatu dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90.
  Ushindi huo unaifanya timu ya kocha Mreno, Jose ifikishe pointi 62 baada ya kucheza mechi 29 na kurejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi, ikiizidi kwa pointi mbili Liverpool inayoteremkia nafasi ya tatu, huku yenyewe ikizidiwa pointi 16 na vinara, Manchester City PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATOKA NYUMA KWA 2-0 NA KUIBAMIZA CRYSTAL PALACE 3-2 'KIAJABU AJABU' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top