• HABARI MPYA

  Sunday, March 04, 2018

  BEKI WA FIORENTINA AFARIKI DUNIA USINGIZINI, SERIE A YASIMAMA

  NAHODHA wa Fiorentina, Davide Astori amefariki dunia akiwa usingizini usiku wa kuamkia leo kuelekea mechi ya Serie A dhidi ya Udinese leo.
  Astori, mwenye umri wa miaka 31, beki wa kimataifa wa Italia, amekuwa na klabu hiyo tangu mwaka 2016 baada ya awali kuchezea timu za Milan, Cagliari na Roma.
  Amefarolo akiwa ameichezea mechi 14 Italia na alikuwemo kwenye kikosi kilichocheza Kombe la Mabara la FIFA mwaka 2013.
  Mechi zote za leo za Serie A zimefutwa ili kumpa heshima mchezaji huyo. 

  Davide Astori amefariki dunia akiwa usingizini usiku wa kuamkia leo kuelekea mechi ya Serie A dhidi ya Udinese leo 


  MECHI ZA SERIE A ZILIZOAHIRISHWA  

  Genoa vs Cagliari
  Atalanta vs Sampdoria
  Benevento vs Hellas Verona
  Chievo vs Sassuolo
  Torino vs Crotone
  Udinese vs Fiorentina
  Milan vs Inter Milan 
  Taarifa nchini zimesema kwamba wachezaji wenzake walikwenda kuvunja mlango wake baada ya Astori kutoteremka kwa ajili ya chai na pia kutopokea simu yake.
  "Jamaa hakutokea kunywa chai Saa 3.30 asubuhi na kwa kawaida alikuwa anakuwa wa kwanza kufika,"amesema Msemaji wa Fiorentina, Arturo Mastronardi.
  "Hivyo walikwenda kumuangalia. Davide alikuwa amelala chumbani yeye mwenyewe. Bado hatujajua sababu za kifo chake. Hakimu alikuja hapa na mwili umechukuliwa uchunguzi, ambao nafikiri utafanyika leo. Hatuna taarifa zaidi,".
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI WA FIORENTINA AFARIKI DUNIA USINGIZINI, SERIE A YASIMAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top