• HABARI MPYA

  Monday, January 15, 2018

  NJOMBE MJI YAIDONDOSHA KAGERA SUGAR SABA SABA

  Na Mwandishi Wetu, NJOMBE
  BAO pekee la Ditram Nchimbi kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili, limewapa wenyeji Njombe Mji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Saba Saba jioni ya leo.
  Ushindi huo wa pili tu kwao msimu huu, unawafanya Njombe Mji FC wafikishe pointi 11 baada ya kucheza mechi 13, ingawa wanaendelea kubaki nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya timu 16.  
  Kagera Sugar wao kwa kupoteza mechi ya leo, wanabaki nafasi ya 10 kwa pointi zao 12 baada ya kucheza mechi 13 pia.
  Ligi Kuu itaendelea Jumatano kwa mabingwa watetezi, Yanga SC kuwakaribisha Mwadui FC ya Shinyanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mzunguko wa 13 utahitimishwa kwa michezo miwili Januari 18, Simba wakiikaribisha Singida United Uwanja wa Taifa na Maji Maji wakiwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NJOMBE MJI YAIDONDOSHA KAGERA SUGAR SABA SABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top