• HABARI MPYA

  Wednesday, January 17, 2018

  MWADUI KUIVAA YANGA BILA ‘FUNDI’ HASSAN KABUNDA LEO DAR

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mwadui FC leo itawakosa nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza akliwemo kiungo Hassan Salum Kabunda ambaye ni majeruhi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Yanga SC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Mwadui FC, Ramadhani Kilao ameiambia Bin Zubeiry Sport – Online kwamba pamoja na Kabunda, timu yake itawakosa pia beki Abdalah Mfuko na mshambuliaji Salim Khamis ambao pia ni majeruhi.
  Kilao amesema kwamba pamoja na kukosekan kwa nyota hao, Kocha Mkuu Mnyarwanda Ali Bizimungu amewanda wachezaji wa kuziba nafasi hizo, ambao ni Awesu Ali Awesu, Joram Mgeveke na Evaristus Bernard Mwanjuki. 
  Mtaalamu Hassan Kabunda hatakuwepo leo, lakini nafasi yake itazibwa na Awesu Ali

  “Nafasi ya Kabunda itazibwa na Awesu, nafasi ya Mfuko itazibwa na Mgeveke na nafasi ya Salim Khamis atacheza Mwanjuki. Na ninaamini kabisa watu watasahu kama kuna watu leo hawapo Mwadui,”amesema.
  Kilao amesema timu yake iliwasili Dar es Salaam juzi na kuweka kambi Magomeni kabla ya jana kufanya mazoezi Uwanja wa Uhuru tayari kabisa kwa mchezo wa leo.
  Na Kilao amesema kwamba wanataka kuvunja mwiko wa kutoifunga Yanga katika mchezo wa leo kwa sababu vijana wake wapo vizuri na maandalizi yamekuwa mazuri.
  Ligi Kuu inaendelea leo kwa mchezo huo mmoja, mabingwa watetezi, Yanga SC wakiwakaribisha Mwadui FC wakati mzunguko wa 13 utahitimishwa kwa michezo miwili kesho, Simba wakiikaribisha Singida United Uwanja wa Uhuru na Maji Maji wakiwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI KUIVAA YANGA BILA ‘FUNDI’ HASSAN KABUNDA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top