• HABARI MPYA

  Thursday, January 11, 2018

  MESSI AZAWADIWA KIATU KILICHOBEBA HISTORIA YA MAISHA YAKE

  HISTORIA ya kusisimua ya maisha ya Lionel Messi kutoka Argentina hadi Barcelona imesimuliwa kwenye pea ya kiatu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amepatiwa zawadi ya kiatu na msanii wa Paraguay kilichobeba historia ya maisha yake.
  Lili Cantero amekuwa akivutiwa mno na maisha ya Messi na mafanikio yake kiasi kwamba akaamua kuchukua muda wake kubuni zawadi nzuri ya kumpa.
  Kiatu hicho kimepambwa na picha za kuanzia Messi yuko mdogo Amerika Kusini, picha za familia yake akiwa na mkewe, Antonella Roccuzzo na amewashika watoto wake, Thiago na Mateo.
  Lionel Messi akiwa ameshika kiatu alichozawadiwa chenye historia a maisha yake PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Msanii huyo ameelezea zaidi kuhusu viatu hivyo akisema kwamba hayo ni matokeo ya kazi ngumu anayoifanya Messi inavyomlipa. "Viatu hivyo vilipelekwa Barcelona kama zawadi kwa mchezaji huyo, kikiwa kimechorwa chote,".
  "Kiatu hicho kinazungumzia maisha ya Messi, kikiwa kimepambwa kwa picha za historia yakena namna alivyojituma kufikia mafanikio,". 
  Kutoka Paraguay na upendo Love, kwa dunia.  
  Messi si mwanasoka wa kwanza kukabidhiwa viatu vilivyochirwa hivyo kutoka kwa msanii huyo mwenyeb kipaji.
  Mwanasoka wa kimataifa wa Paraguay, Derlis Gonzalez wa klabu ya Dynamo Kiev pia ni miongoni mwa wachezaji wengine waliowahi kupewa zawadi hiyo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AZAWADIWA KIATU KILICHOBEBA HISTORIA YA MAISHA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top