• HABARI MPYA

  Wednesday, December 06, 2017

  YANGA NA SIMBA WAPATA VIBONDE KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA watetezi, Simba SC watamenyana na Green Worriers, zote za Dar es Salaam katika mchezo wa Raundi ya Pili ya Kombe la Azam Sports Federation kati ya Desemba 20 na 25 mwaka huu Jijini.
  Mahasimu wao, Yanga watamenyana na Reha FC katika hatua hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 64, wakati Azam FC watamenyana na Area C ya Dodoma Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
  Katika droo iliyopangwa leo studio za Azam TV, Tabata mjini Dar es Salaam, ikiongozwa na wachezaji nyota wa zamani nchini, makipa Steven Nemes, Mwameja Mohammed, beki Kenneth Mkapa na mshambuliaji Bitta John, washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC watamenyana na Makanayagio FC ya Rukwa.
  Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Madini FC, Abajalo wataikaribisha Tanzania Prisons, Njombe Mji wataikaribisha Mji Mkuu, Boda Boda FC ya Arusha watakuwa wenyeji wa Singida United na Mwadui FC wataikaribisha Pepsi FC.
  Gwiji wa soka nchini, Kenneth Pius Mkapa (kushoto) akionyesha karatasi inayomtambulisha mpinzani wa Yanga, Reha FC. Kulia ni gwiji mwingine, Bitta John aliyeichagua Yanga
  Makipa maarufu wa zamani, Mohammed Mwameja (kulia) na Steven Nemes (kushoto)
  Wadau waliohudhuria droo hiyo leo studio za Azam Sports 2 

  RATIBA KAMILI RAUNDI YA PILI AZAM SPORTS FEDERATION CUP
  Ruvu Shooting Vs Madini FC 
  Abajalo Vs Tanzania Prisons
  Njombe Mji Vs Mji Mkuu
  Singida United Vs BodaBoda
  Mwadui FC Vs Pepsi
  Maji Maji FC Vs New Generation
  Boma FC Vs Ndanda FC
  Stand United Vs AFC Arusha
  Burkina Faso FC Vs Lipuli FC
  Green Worriers Vs Simba SC
  Azam FC Vs Area C
  Yanga SC Vs Reha FC
  Mbeya City Vs Ihefu
  Villa Squad Vs Mtibwa Sugar
  Kagera Sugar Vs Makambako
  Makanayagio Vs Mbao FC 
  JKT Mlale Vs KMC
  Ambassador Vs JKT Oljoro
  Mshikamano Vs Polisi Tanzania
  Rhino Vs Alliance 
  Ashanti United Vs Friends Rangers
  Toto Africans Vs Eleven Stars
  Maji Maji Rangers Vs Mbeya Kwanza
  Milambo FC Vs Buseresere FC
  African Lyon Vs Kiluvya United
  Biashara United Vs Mawenzi Market
  Mvuvumwa Vs JKT Ruvu
  Coastal Union Vs Dodoma FC
  Polisi Dar Vs Mgambo JKT
  Kariakoo United Vs Transit Camp
  Shupavu Vs Real Moja Moja
  Mufindi FC Vs Pamba SC 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA SIMBA WAPATA VIBONDE KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top