• HABARI MPYA

  Saturday, December 17, 2016

  ZAMBIA BINGWA COSAFA U-20, WAILAZA AFRIKA KUSINI 2-1

  ZAMBIA imetwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za kusini mwa Afrika COSAFA U20 baada ya kuifunga Afrika Kusini mabao 2-1 jana.
  Young Chipolopolo walipata bao lao la kwazna dakika ya nane kupitian kwa Kenneth Kalunga akimalizia pasi ya Enock Mwepu.
  Amajita wakatengeneza nafasi nyingi lakini wakashindwa kuzitumia ikiwemo nzuri zaidi ya Sipho Mbule aliyepaisha.
  Hata hivyo, Waafrika Kusini wakasawazisha dakika ya 41 wakati Kabelo Seriba akimalizia mpira wa adhabu wa Luther Signh.
  Kipindi cha pili, Paston Daka alikaribia kuifungia timu yake bao la pili kama si kazi nzuri ya beki wa Amajitas, Trecious Malepe kuokoa huku akiwa kwenye mstari wa goli kuikatalia bao la wazi Chipolopolo.
  Wazambia wakaendelea kusukuma mashambulizi hadi wakafanikiwa kupata bao la pili na la ushindi zikiwa zimebaki dakika tano kutokana na jitihada za Boyd Musonda aliyewakusanya mabeki wa wenyeji kutokea nje ya boksi kabla ya kumtungua Sanele Tsabalala.
  Katika dakika za majeruhi, Wazambia walirudi nyuma kulinda lango lao  na kuwazuia kabisa Afrika Kusini kupata bao la kusawazisha.
  Vikosi vilikuwa; Afrika Kusini: Sanele Tshabalala, Reeve Frosler, Repo Melepe, Kabelo Seriba, Aghmat Ceres, Wiseman Meyiwa, Sibongakonke Mbatha, Luther Singh, Nkosingiphile Ngcobo, Sipho Mbule na Menzi Ndwandwe.
  Zambia: Mangani Banda, Moses Nyondo, Prosper Chiluya, Solomon Sakala, Chrispine Sakulanda, Fashion Sakala, Enock Mwepu, Shemmy Mayembe, Edward Chilufya, Body Musonda na Patson Daka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAMBIA BINGWA COSAFA U-20, WAILAZA AFRIKA KUSINI 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top