• HABARI MPYA

  Sunday, December 11, 2016

  TFF YAWAOMBA WANANCHI KUPENDEKEZA MAJINA YA TIMU ZA TAIFA U-23

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetoa nafasi kwa wafamilia wa soka kupendekeza majina ya timu za Taifa za vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 za wanawake na wanaume.
  Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari jana ilisema kwamba timu hizo za taifa ya wanawake na wanaume U-23, zitaingia kwenye programu ya kuandaliwa kuwania nafasi ya kucheza fainali za michuano ya Olimpiki zitazayofanyika jijini Tokyo, Japan; mwaka 2020.
  Wadau wa mpira wa miguu nchini wameombwa kupendekeza majina hayo kupitia anwani za tanfootball@tff.or.tz, mjselestine@yahoo.co.uk au Namba za simu +255 678 297727, +255 624 121812, +255-22-2182032 au nukunishi (faksi) +255-22-2182031.
  Tayari Tanzania ina majina ya timu za Taifa ya wanaume wakubwa (Senior National Team) ambayo ni Taifa Stars, Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania ‘Twiga Stars’ na Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’.
  Zimo pia timu ya Taifa ya Vijana ya wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’; Timu ya Taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘The Tanzanite Queens’ na timu ya Taifa ya Vijana ya wenye umri wa chini ya mika 17 ‘Serengeti Boys’
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAWAOMBA WANANCHI KUPENDEKEZA MAJINA YA TIMU ZA TAIFA U-23 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top