• HABARI MPYA

  Friday, December 02, 2016

  NGASSA: MIMI BADO MCHEZAJI HALALI WA FANJA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba yeye ni mchezaji halali wa Fanja ya Oman na alirejea nyumbani kwa ruhusa maalum.
  Aidha, Mrisho Ngassa ameshangazwa na habari kwamba yeye amesaini Mbeya City na akasema alikutana na Ofisa Habari wa timu hiyo, Dismass Ten katika mazungumzo ya kawaida na haikuhusu usajili.
  “Alinipigia simu Ofisa Habari wa Mbeya City, tunafahamiana. Tukakutana kwa mazungumzo na kupiga picha tukiwa kwenye mgahawa. Baada ya hapo tukaachana, sijasaini Mbeya City,”alisema.
  Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba yeye ni mchezaji halali wa Fanja ya Oman na alirejea nyumbani kwa ruhusa maalum

  Ngassa alisema kwamba yeye kama mchezaji soka ni ajira yake na anaamini anaweza kucheza popote wakati wowote, lakini haipendezi kuandikwa mambo ambayo si ya kweli juu yake.
  “Inakuwa vizuri inapoandikwa nimesaini timu, wakati nimesaini kweli. Lakini si kusema nimesaini Mbeya City wakati sijasaini. Naiheshimu Mbeya City. Ni timu nzuri na napenda kuichezea siku moja hususan kwa sababu kocha wao, (Kinnah Phiri) nimewahi kufanya naye kazi. Lakini itakuwa vizuri iandikwe nimesaini wakati nimesaini. Kwa sasa napenda ieleweke sijasaini,”alisema.
  Mchezaji huyo wa zamani wa Azam, Simba na Yanga amesema tayari amekwishakamilisha kilichomrudisha nyumbani na sasa anasubiri kutumiwa tiketi arudi kazini Oman.
  “Mimi nilikuja huku kwa ruhusa maalum kwa ajili ya mambo ya kifamilia. Na baada ya kukamilisha mambo yangu, nimewatumia taarifa Fanja ili wanitumie tiketi nirejee kazini, kwa hiyo ninawasubiri wao,”alisema Ngassa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA: MIMI BADO MCHEZAJI HALALI WA FANJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top