• HABARI MPYA

  Saturday, May 06, 2023

  LIVERPOOL YAICHAPA BRENTFORD 1-0 ANFIELD BAO LA SALAH


  WENYEJI, Liverpool FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Bao pekee la Wekundu hao limefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, Mohamed Salah dakika ya 13, akimalizia pasi ya beki Mholanzi, Virgil van Dijk.
  Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mjerumani, Jurgen Klopp inafikisha pointi 59 na kusogea nafasi ya tano, wakati Brentford inabaki na pointi zake 50 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 34.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA BRENTFORD 1-0 ANFIELD BAO LA SALAH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top