• HABARI MPYA

  Monday, August 01, 2022

  KIDUNDA AMCHAPA KATOMPA, ATWAA UBINGWA WA WBF

  BONDIA Suleiman Kidunda juzi alipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya ushindi wa pointi dhidi ya Erick Tshimanga Katompa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kutwaa ubingwa wa WBF Intercontinental uzito wa Super Middle katika pambano lililofanyika Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Katika mapambano ya utangulizi,mkongwe Shaaban Kaoneka alimchapa kwa Knockout Karim Mandonga. Aidha,George Bonabucha alimchapa Yusuph Ally wa Malawi kwa pointi. Naye mwanamuziki aliyehamia kwenye ndondi,Khalid Chokoraa alitoka droo na Chiddy Benga Naye Ezra Paul alimchapa Shaffi Mohamed kwa Knockout.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIDUNDA AMCHAPA KATOMPA, ATWAA UBINGWA WA WBF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top