• HABARI MPYA

        Monday, November 09, 2020

        CHILUNDA AJIUNGA NA MOGHREB ATLETICO TETUAN YA MOROCCO KWA MKATABA WA MIAKA MITATU

        Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
        ALIYEKUWA mshambuliaji wa Azam FC, Shaaban Iddi Chilunda, amekamilisha uhamisho wa kujiunga na miamba ya Morocco, Moghreb Atletico Tetuan kwa mkataba wa miaka mitatu.
        Chilunda anakwenda kuungana na Mtanzania mwingine, kiungo Maka Edward Mwasomola aliyejiunga na klabu hiyo mwaka jana kwa mkataba wa miaka minne kutoka Yanga SC ya Dar es Salaam pia.
        Awali Chilunda ilikuwa ajiunge na Mouloudia Oudja ya huko, lakini imeshindakana baada ya baadhi ya taratibu kushindikana kabla ya Azam FC kumalizana na Tetuan.
        Shaaban Chilunda amejiunga na miamba ya Morocco, Moghreb Atletico Tetuan kwa mkataba wa miaka mitatu 


        Mshambuliaji huyo anakuwa mchezaji wa pili wa Azam FCetu kuondoka msimu huu kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi baada ya Novatus Dismas, kujiunga na vigogo wa Israel, Maccabi Tel-Aviv.
        Wachezaji wote wawili wamekulia kwenye kituo cha kukuza vipaji cha Azam FC Academy.
        Mwaka juzi, Azam FC ikifanya biashara nyingine ya kumuuza nshambuliaji wake kinda, Yahya Zayd, kwenda kwa miamba ya Misri, Ismailia.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: CHILUNDA AJIUNGA NA MOGHREB ATLETICO TETUAN YA MOROCCO KWA MKATABA WA MIAKA MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry