• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 12, 2020

  SEVILLA YAITOA WOLVES, KUKUTANA NA MAN UNITED

  BAO pekee la Lucas Ocampos dakika ya 88 limeipeleka Sevilla Nusu Fainali ya UEFA Europa League baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Schauinsland-Reisen-Arena Jijini Duisburg, Ujerumani na sasa itakutana na Manchester United katika Nusu Fanali Jumapili ya Agosti 16.
  Wolves watajilaumu wenyewe kutokana na mshambuliaji wao, Raul Jimenez kukosa penalty iliyookolewa na ma kipa wa Sevilla, Bono kufuatia Adama Traore kuangushwa kwenye boksi.
  Nayo Shakhtar Donetsk ikaibua na ushsindi wa 4-1 dhidi ya FC Basel katika Robo fainali nyingine Uwanja wa VELTINS-Arena Jijini Gelsenkirchen na sasa itakutana na Inter Milan katika Nusu Fainali Jumapili pia. PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Search Results

  Web rSha

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SEVILLA YAITOA WOLVES, KUKUTANA NA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top