• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 02, 2020

  YARMOLENKO APIGA LA USHINDI WEST HAM YAICHAPA CHELSEA 3-2

  Andriy Yarmolenko akishangilia baada ya kuifungia West Ham United bao la ushindi dakika ya 89 ikiwalaza Chelsea 3-2 Uwanja wa London katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Mabao mengine ya West Ham yalifungwa na Tomas Soucek dakika ya 45 na ushei na Michail Antonio dakika ya 51, wakati ya Chelsea yote yalifungwa na Willian dakika ya 42 kwa penalti na 72.
  Pamoja na kufungwa, Chelsea wanabaki nafasi ya nne na pointi zao 54, sasa wakiizidi pointi mbili tu Manchester United baada ya wote kucheza mechi 32.
  Tayari Liverpool ni mabingwa kwa ponti zao 86, wakifuatiwa kwa mbali na Manchester City yenye pointi 63 baada ya wote kucheza mechi 31 na Leicester City pointi 55 za mechi 32 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YARMOLENKO APIGA LA USHINDI WEST HAM YAICHAPA CHELSEA 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top