• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 02, 2020

  SANCHEZ, ASHLEY YOUNG WOTE WAFUNGA INTER MILAN YASHINDA 6-0

  Alexis Sanchez akiifungia Inter Milan bao la pili kwa penalti dakika ya 20 katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Brescia kwenye mchezo wa Serie A usiku wa jana Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan, Mabao mengine ya Inter Milan yalifungwa na Ashley Young dakika ya tano, Danilo D'Ambrosio dakika ya 45, Roberto Gagliardini dakika ya 52, Christian Eriksen dakika ya 83 na Antonio Candreva dakika ya 88 na kwa ushindi huo, timu ya kocha Antonio Conte inafikisha pointi 64, ingawa inabaki nafasi ya tatu, sasa ikizidiwa pointi nne na Lazio, wakiwa nyuma ya Juventus inayoongoza kwa pointi zake 72  baada ya wote kucheza mechi 29 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SANCHEZ, ASHLEY YOUNG WOTE WAFUNGA INTER MILAN YASHINDA 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top