• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 08, 2020

  SADIO MANE ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA

  NYOTA wa Senegal, Sadio Mane ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika kufuatia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Liverpool na kuifikisha timu yake ya taifa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
  Mane mwenye umri wa miaka 27, ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kushika nafasi ya pili mbele ya mchezaji mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah wa Misri miaka ya 2017 na 2018 na kushika nafasi ya tatu mwaka 2016. 
  Anakuwa mchezaji pekee kutoka Senegal kushinda tuzo hiyo baada ya El Hadji Diouf, aliyeshinda mara mbili, mwaka 2001 na 2002.

  Winga wa Senegal, Sadio Mane ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika 

  WASHINDI WOTE WA TUZO ZA CAF 2020 

  Mchezaji Bora wa Kiume wa Mwaka: Sadio Mane
  Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka: Asisat Oshoala
  Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka: Achraf Hakimi
  Timu ya Mwaka: Onana, Aurier, Matip, Koulibaly, Hakimi, Gueye, Mahrez, Zyech, Salah, Aubameyang, Mane
  Goli Bora la Mwaka: Mahrez (mpira wa adhabu Nusu Fainali AFCON)
  Kocha Bora wa Mwaka: Djamel Belmadi
  Kocha Bora wa Kike wa Mwaka: Diseree Ellis
  Timu Bora ya Mwaka: Algeria
  Timu Bora ya Mwaka ya Wanawake: Cameroon
  Mane ameshinda tuzo hiyo baada ya kura zilizopigwa na makocha wakuu, Wakurugenzi wa Ufundi na Manahodha wa timu za taifa za wakubwa kutoka nchi wanachama wa CAF.
  Naye Achraf Hakimi anayecheza kwa mkopo Borussia Dortmund kutoka Real Madrid alishinda tuzo ya Mwanasoka Chipukizi.
  Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka imechukuliwa na  Djamel Belmadi baada ya kuiwezesha Algeria kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.
  Nyota wa Ligi Kuu ya England, Serge Aurier wa Totenham, Joel Matip wa Liverpool, kiungo wa zamani wa Everton, Idrissa Gueue, nyota wa Manchester City, Riyad Mahrez na Nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang wamejumuishwa kwenye Timu ya Mwaka pamoja na Mane na Salah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SADIO MANE ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top