• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 08, 2019

  SIMBA KUCHEZA ‘MECHI YA KIMATAIFA’ JUMAMOSI TAIFA, KUMENYANA NA BANDARI YA MOMBASA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa soka Tanzania, Simba SC Jumamosi watakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bandari ya Mombasa nchini Kenya ambao utafanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
  Simba SC inatumia mapumzuko mafupi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kupisha kalenda ya mechi za kirafiki za kimataifa kwa kukinoa zaidi kikosi chake. 
  Na japokuwa itawakosa nyota wake kadhaa watakochukuliwa na timu zao za taifa, Simba SC itakuwa na mechi tatu jumla kipindi hiki.

  Baada ya kumenyana na Bandari, Wekundu wa Msimbazi watasafiri hadi mkoani Kigoma kwa ajili ya michezo miwili zaidi ya kirafiki.
  Wataanza kumenyana na wenyeji, Mashujaa FC Oktoba 14 kabla ya kucheza na mabingwa wa Burundi,  Aigle Noir FC Oktoba 16, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Lake Tanganyika.
  Katika mechi hizo, Simba SC itawakosa mabeki; Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, viungo Jonas Mkude, Muzamil Yassin na washambuliaji Miraj Athumani ‘Madenge’ ambao wapo Taifa Stars na Meddie Kagere anayekwenda kujiunga na Rwanda ‘Amavubi’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA KUCHEZA ‘MECHI YA KIMATAIFA’ JUMAMOSI TAIFA, KUMENYANA NA BANDARI YA MOMBASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top