• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 29, 2017

  SAMATTA KUIKOSA KAMBI YA TAIFA STARS MISRI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta hatashiriki kambi ya wiki moja ya timu hiyo nchini Misri, na badala yake atajiunga na wenzake Dar es Salaam tayari kwa mchezo dhidi ya Lesotho.
  Taifa Stars watamenyana na Lesotho Juni 10, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.
  Meneja wa Taifa Stars, Danny Msangi ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Samatta hataiwahi kambi ya Misri kwa sababu anakabiliwa na majukumu katika klabu yake, KRC Genk nchini Ubelgiji.
  Msangi amesema kwamba, kiungo Farid Malik Mussa atajiunga na timu nchini Misri akitokea Hispania anakochezea DC Tenerife ya Daraja la Kwanza, ingawa bado anakomazwa kikosi cha pili. 
  Mbwana Samatta hatashiriki kambi ya Taifa Stars nchini Misri kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho

  Kikosi cha wachezaji 21 kinatarajiwa kuondoka kesho kwa ndege ya Ethiopia kwenda Cairo, Misri kwa kambi ya wiki kabla ya kurejea nchini Juni 7 kwa ajili ya mechi dhidi ya Lesotho.
  Kikosi kamili cha Stars ni; Makipa; Aishi Manula (Azam), Benno Kakolanya (Yanga), Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
  Mabeki; Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Yanga), Mwinyi Mngwali (Yanga), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Aggrey Morris (Azam), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam).  
  Viungo; Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Farid Mussa (DC Tenerife, Hispania) na Shiza Kichuya (Simba).
  Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (FC Eskilstuna, Denmark), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar), Ibrahim Hajib (Simba) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).
  Ikumbukwe Mayanga anasaidiwa na Fulgence Novatus, kocha wa makipa, Patrick Mwangata, Meneja Dani Msangi, Madaktari Gilberti Kigadiya na Richard Yomba pamoja na mtunza vifaa Ally Ruvu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA KUIKOSA KAMBI YA TAIFA STARS MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top