• HABARI MPYA

    Tuesday, May 30, 2017

    NI MWAKA MMOJA TANGU BIN ZUBEIRY IWE TOVUTI RASMI

    MAPEMA mwaka 2012, tasniya ya Habari ilipata ugeni wa chombo kipya rasmi cha habari mtandaoni, bongostaz.blogspot.com ambacho kilikuwa maalum kwa habari za michezo, sanaa na burudani.
    Bogostaz ilijikita zaidi kwenye habari za soka, ikiripoti kwa weledi, usawa na kwa ujumla kuzingatia miiko ya taaluma ya Uandishi wa Habari.
    Na hiyo ni kwa sababu, mwanzilishi na mmiliki wake, Mahmoud Ramadhani Zubeiry ni Mwandishi wa Habari halisi, aliyepitia mikononi mwa magwiji wa taaluma ya Habari akina Jenerali Twaha Ulimwengu, Salva Rweyemamu, Johnson Mbwambwo, Francis Chirwa na wengine waliompika akaiva kitaaluma.
    Mtendaji Mkuu wa Bin Zubeiry Sports - Online anawapa '5' wasomaji wote wa tovuti hii  
    Na hivi ndivyo Bin Zubeiry Sports - Online inavyosomwa, watu zaidi ya 100,000 wanaingia kila siku mfululilizo

    Bongostaz ilijitahidi kuwa ya kipekee, kwanza kuanzisha mfumo wa kupandisha habari kila wakati, kila siku, kutoka mfumo uliokuwapo wakati huo wa kupandisha habari wenye chombo chao wakijisikia, wakati mwingine hata wiki nzima ilipita bila habari au taarifa mpya.
    Changamoto hiyo ikapokewa vizuri na vyombo vya habari vya mitandaoni tulivyovikuta, ikiwemo Michuzi Blog ya mkubwa wetu na mwasisi wa mambo haya ya habari za mitandaoni nchini, Muhiddin Issa Michuzi na nyinginezo.
    Bongostaz haikusita kutumia gharama yoyote katika kuhakikisha inapata habari, iwe ndani au nje ya nchi na kwa sababu hiyo ndani ya muda mfupi, hiyo ikawa blogu namba moja ya michezo Tanzania.
    Malaki wana Like habari za Bin Zubeiry Sports - Online kwenye ukurasa wetu wa Facebook
    Malaki wana Like habari za Bin Zubeiry Sports - Online kwenye ukurasa wetu wa Facebook 
    Malaki wana Like habari za Bin Zubeiry Sports - Online kwenye ukurasa wetu wa Facebook
    Hata habari za Ulaya na mataifa mengine mbalimbali zina mashiko nani ya Bin Zubeiry
    1.1 K inaonekana hapo watu wame Like habari kuhusu Ndikumana
    Zaidi ya watu 120,000 wame Like ukurasa wetu wa Faceboob

    Ujio wa blogu nyingine za michezo zilizokuja na sera tofauti zikiwemo zisizozingatia miiko na maadili ya Taaluma ya Habari zaidi ya maslahi, haukuiyumbisha Bongostaz na ikabaki kusimama kama chombo mfano wa kuigwa cha habari za mitandaoni.
    Tumepitia vipindi tofauti na katika kukuwa kwetu kama taasisi, tulilazimika kuongeza wafanyakazi, na kuna wakati tulijikuta tunaajiri watu wasio waadilifu, waaminifu na wakataka kuchafua sifa ya chombo chetu.
    Lakini tulisimama imara na kuiaminisha jamii kilichotokea ni bahati mbaya, kwa kuhakikisha kila asiyestahili katika safari yetu tunamteremsha jahazini. Na ndivyo ilivyofanyika na watu wakaendelea kuwa na imani nasi.
    Wakati mwingine zilifanyika mbinu chafu za watu wenye roho mbaya kujaribu kutaka kuishusha Bongostaz, kwa kuwachafua baadhi yetu akiwemo Mtendaji Wetu Mkuu, Mahmoud Zubeiry – lakini hekima na busara vilituongoza kustahmili na kupuuza maudhi yote, huku tukiendelea na uwajibikaji wetu mzuri uso na shaka.
    Ukawadia wakati, Mei mwaka jana tukaamua kutoka kwenye blogu na kuwa tovuti rasmi ya habari za michezo, www.binzubeiry.co.tz maarufu kama Bin Zubeiry Sports – Online na sasa umetimia mwaka mmoja.
    Ni mafanikio makubwa kwa mwonekano wa ndani na nje – Bin Zubeiry Sports – Online ni kitu kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi. Kila kitu kinajieleza chenyewe kuhusu sisi, kama mtu mmoja mmoja na kama taasisi.
    Hatuna cha kusema zaidi ya kwanza kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha na pili kwenu nyinyi wasomaji wetu kwa namna mlivyotuamini na heshima kubwa mliyotupa. Tunashukuru sana.
    Bin Zubeiry Sports – Online kwa sasa tunajivunia kuwa tovuti bora zaidi ya habari za michezo kwa lugha ya Kiswahili duniani.
    Tunajivunia siyo tu kutangaza kwa wingi habari za michezo za nyumbani na wachezaji wetu hususan soka, lakini pia kukitangaza Kiswahili, lugha yetu mwanana.
    Pamoja na hayo, Bin Zubeiry Sports – Online hatutaelewa sifa kwa mafanikio ya awali, bali tutaendelea kusimamia dhamira tulizojiwekea ili kuendelea kuwa bora kwa vitendo, kwa maana zote na sifa zote njema.
    Tunawashukuru kwa kutuamini na kuendelea kuwa nasi, na tunaomba muendelee kutuamini, kwani mambo mazuri zaidi yanakuja. Asanteni.  Furahia mwaka mmoja wa Bin Zubeiry Sports – Online. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI MWAKA MMOJA TANGU BIN ZUBEIRY IWE TOVUTI RASMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top