• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 26, 2017

  BINGWA KOMBE LA AZAM SPORTS KUVUNA MILIONI 50 KESHO

  Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
  BINGWA wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ijulikanayo pia kama Azam Sports Federation Cup atajinyakulia kitita cha Sh. Milioni 50 kutoka kwa wadhamini, Azam TV.
  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema leo kwamba mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kesho baina ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza itaanza saa 10.00 jioni.
  Lucas amesema bingwa wa ASFC ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
  Katika hatua nyingine, Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino juzi alituma ujumbe TFF kuipongeza klabu ya Yanga ya Dar es Salaam kwa kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.
  Yanga imetwaa Kombe hilo ikiwa ni mara tatu mfululizo na katika salamu za pongezi, Rais Gianni Infantino amesema ubingwa huo wa Young Africans ni kielelezo cha ushirikiano baina ya wachezaji, kocha, utawala, matabibu pamoja na mashabiki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BINGWA KOMBE LA AZAM SPORTS KUVUNA MILIONI 50 KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top