• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 22, 2017

  MALINZI: MSUVA, MUSSA WOTE WAFUNGAJI BORA NA WATAPATA ZAWADI SAWA

  Na Mwandishi Wetu, LIBREVILLE
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kwamba wachezaji Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga waliofungana kwa mabao baada ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wote watapata zawadi.
  Akizungumza leo mjini Libreville, Malinzi ambaye alikuwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 kwenye Fainali za Afrika, amesema Mussa na Msuva kila mmoja atapata nusu ya Sh. Milioni 5.8 baada ya kumaliza na mabao 14.  
  Simon Msuva wa Yanga (kulia) atapata zawadi sawa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting baada ya kufungana naye kwa mabao Ligi Kuu  

  “Kwa kuwa vijana wetu Abdulrahman Mussa na Simon Msuva wamefungana kwa mabao katika Ligi Kuu (kila mmoja 14), wote ni wafungaji bora na watapewa zawadi sawa (kutoka) Sh. Milioni 5.8,”amesema.
  Ligi Kuu imefikia tamati Jumamosi kwa Yanga kutetea ubingwa, Simba nafasi ya pili na Kagera Sugar nafasi ya tatu, huku JKT Ruvu, African Lyon na Toto Africans zikiteremka daraja.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINZI: MSUVA, MUSSA WOTE WAFUNGAJI BORA NA WATAPATA ZAWADI SAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top