• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 28, 2017

  SIMBA NA MBAO FC KATIKA PICHA JANA UWANJA WA JAMHURI

  Beki wa Mbao FC ya Mwanza, David Mwasa akipiga mpira dhidi ya mshambuliaji wa Simba SC ya Dar es Salaam, Mrundi Laudit Mavugo katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) jana Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Simba ilishinda 2-1 
  Beki wa Mbao FC, Boniphace Maganga akilala chini kuondoa mpira miguuni mwa beki wa Simba, Abdi Banda 
  Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib akikimbilia mpira dhidi ya beki wa Mbao, Boniphace Maganga 
  Kipa wa Mbao FC, Benedict Haule (kushoto) akitoka langoni mwake kuokoa dhidi ya kiungo wa Simba, Muzamil Yassin (kulia) huku wake, David Mwasa naye akisaidia
  Mshambuliaji wa Simba, Muivory Coast, Frederick Blagnon akipambana katikati ya wachezaji wa Mbao FC, Youssouf Ndikumana (kulia) na Asante Kwasi (kushoto)
  Jamal Mwambeleko wa Mbao FC (kulia) akimiliki mpira mbele ya Muzamil Yassin wa Simba (kushoto)
  Youssouf Ndikumana wa Mbao akiondoka na mpira mbele ya Mrundi mwenzake, Laudit Mavugo wa Simba
  Kiungo wa Simba, Said Ndemla akiwa na mpira katikati ya wachezaji wa Mbao
  Kikosi cha Mbao FC jana Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na chini ni kikosi cha Simba

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA MBAO FC KATIKA PICHA JANA UWANJA WA JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top