• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 23, 2017

  SERENGETI BOYS WAONDOKA LEO USIKU GABON

  Na Mahmoud Zubeiry, LIBREVILLE
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ijulikanayo kwa jina la utani la Serengeti Boys inatarajiwa kuondoka mjini hapa Saa 7.15 usiku wa leo kurejea nyumbani, Dar es Salaam baada ya kutolewa kwenye Fainali za Vijana Afrika juzi.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ambaye yuko na timu hiyo mjini hapa, amesema kwamba Serengeti Boys inatarajiwa kuingia Dar es Salaam Saa 8.50 mchana wa kesho na moja kwa moja kwenda kambini, hoteli ya Urban iliyopo katikati ya jiji kwa ajili ya kuagwa.
  Beki wa kushoto wa Serengeti Boys, Nickson Kibabage akiwa amepigwa butwaa baada ya mechi Jumapili
  Serengeti ilitolewa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, baada ya kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Jumapili Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, Gabon.
  Matokeo hayo yalizifanya Niger na Tanzania zifungane pointi na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo mshindi katika mechi baina yao akafuzu Kombe la Dunia Oktoba mwaka huu India na pia kwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo.
  Niger imeungana na Mali iliyoongoza kundi kwa pointi zake saba, baada ya ushindi wa mechi mbili na sare moja, wakati Tanzania na Angola zote zimetolewa. Timu nyingine zilizofuzu Nusu Fainali ni Ghana na Guinea kutoka Kundi A. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS WAONDOKA LEO USIKU GABON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top