• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 31, 2017

  KIPA MCAMEROON WA LYON AWAITA YANGA MEZANI WAKAMILISHE DILI AKAPIGE MZIGO JANGWANI

  Na Kambwili Ntalia, DAR ES SALAAM
  KIPA Youthe Rostand amewaambia viongozi wa Yanga SC waache kumuogopa na wamuite mezani wazungumze kama kweli wana nia ya kumsajili.
  Kumekuwa na tetesi za muda mrefu kwamba kipa huyo Mcameroon ambaye timu yake iliyomleta nchini, African Lyon imeteremka daraja kutoka Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara anatakiwa na Yanga SC. 
  Na akizungumzia na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam, Rostande amesema kwamba uwezekano way eye kubaki African Lyon ni mdogo kwa sababu ni vigumu kwake kuendelea kuchezea timu hiyo baada ya kushuka daraja.
  Youthe Rostand amewaambia viongozi wa Yanga SC wamuite mezani wazungumze kama kweli wanamtaka 

  “Kwa sasa naangali uwezekano wa kupata timu ya Ligi Kuu, ili nijiunge nayo, lakini kubaki Lyon baada ya kushuka daraja ni ngumu,”amesemaa. 
  Hata hivyo, Rostande ameshangaa kusikia kwa muda mrefu kwamba  anatakiwa na mabingwa wa Ligti Kuu nchini, Yanga lakini wanasita kumuita kwa mazungumzo yoyote na yeye hivyo kama wana nia na huduma yake wafike mezani wazungumze.
  "Sizani kama nitacheza ligi ya chini zaidi ya hapa, inabidi itambulike kuwa nimeshamaliza mkataba na timu hii hivyo ni rahisi kwangu mimi kupata timu nyingine ya ligi na nina imani nitazipata tu,"alisema.
  "Mimi hakuna klabu ambayo imefika mezani kuzungumza na mimi masuala ya kimkataba hata hao Yanga hawajafika, kwa hiyo kama kuna timu inanihitaji basi wafike mezani tuzungumze tukikubaliana nitasaini lakini iwe ya ligi kuu,"alisema.
  Africa Lyon inaweza kupoteza wachezaji wake wengi nyota baada ya kushuka daraja  na tayari klabu mbalimbali za Ligi Kuu zimeonyesha nia ya dhati ya kuwachukua wachezaji hodari wa timu hiyo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPA MCAMEROON WA LYON AWAITA YANGA MEZANI WAKAMILISHE DILI AKAPIGE MZIGO JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top