• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 26, 2017

  RONALDO MATATANI KWA TUHUMA ZA KUKWEPA KODI HISPANIA

  WAENDESHA mashitaka nchini Hispania wanatafakari kuhusu kumfungulia mashitaka Cristiano Ronaldo kwa ukwepaji wa kodi kiasi cha Euro Milioni 15 kati ya mwaka 2011 na 2014.
  Waendesha mashitaka walisema Alhamisi kwamba wanajipa hadi mwishoni mwa Juni kuamua juu ya nyota huyo wa Real Madrid, kulingana na ushahidi uliopatikana kutokana na uchunguzi wa Maofisa kodi.
  Maofisa kodi wamesema Ronaldo alirekebisha madeni yake ya kodi na kulipa Milioni 6 zaidi, lakini ofisi ya kodi inaamini angelipa Euro Milioni 15 zaidi.
  Ronaldo ameposti picha hii akiwa na mpenzi wake Georgina Rodriguez kwenye ukurasa wake wa Instagram  

  Ofisi ya Kodi imewaagiza waendesha mashitaka kumfungulia mashitaka Ronaldo kwa kukwepa kodi na kupendekeza afungwe jela japo miaka mitano.  
  Waendesha mashitaka hao wamesema kwamba kama wataamua kumfungulia mashitaka, na ikiwa Nahodha huyo wa Ureno atakutwa na hatia na mahakama, atahukumiwa kifungo jela kwa miezi isiyopungua 15, ingawa hatakwenda jela kwa kuwa hilo ni kosa lake la kwanza. 
  Mawakala wa Ronaldo wamekanusha madai hayo na wamesema kijana huyo wa umei wa miaka 32 amelipa kwa ukamilifu kodi zake. 
  Mkali huyo wa mabao wa Real Madrid ameonekana kuzipuuza habari hizo na kujiweka karibu na mpenzi wake Georgina Rodriguez kwa mujibu wa picha aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram unaofuatiliwa na watu Milioni 102.
  Ronaldo ameweka picha hiyo na vikorombwezo vya kimapenzi kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi dhidi ya Juventus.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO MATATANI KWA TUHUMA ZA KUKWEPA KODI HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top