• HABARI MPYA

  Tuesday, May 23, 2017

  GRIEZMANN ASEMA KUTUA MAN UNITED NI "6 KWA 10

  MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amedokezea uelekeo wake Manchester United akisema zimebaki hatua nne za kukaribia Old Trafford kati ya 10.
  Bin Zubeiry Sports - Online mara kadhaa imeandika juu ya nyota huyo wa Ufaransa ambaye dili lake linaweza kugharimu Pauni Milioni 155 likihusisha ada ya uhamisho na mshahara kwa miaka mitano inayopendekezwa kutakiwa United.
  Griezmann anatarajiwa kuwa mmoia wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa Ligi Kuu England, kiasi cha Pauni 295,000 kwa wiki na uhamisho wake unaweza kugharimu Pauni Milioni 80 kutoka klabu hiyo ya Hispania. Griezmann, mwenye umri wa miaka 26, amesema; "Nafikiri mustakabali wangu utaamuliwa wiki mbili zijazo,".


  Antoine Griezmann amesema yuko karibuni kabisa kujiunga na Manchester United
   
  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  Alipoulizwa kama United ndiyo kitakuwa kituo chake kifuatacho, akasema; "Inawezekana. Naweza kukupa uhakika wa sita kati ya 10,".
  Na kuhusu kubaki Atletico Madrid, Griezmann akasema: "Kuna saba kati ya 10 ya nafasi ya kubaki,". 
  Inafahamika ushindi kwa United dhidi ya Ajax katika fainali ya Europa League utawahakikishia nafasi katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao, hivyo watajiongezea nafasi za kumpata mchezaji huyo. 
  Griezmann, anayevaa jezi namba 7 Atletico na timu ya taifa ya Ufaransa, pia alizungumzia namna anavyovutiwa na gwiji wa zamani wa Manchester United na England, mvaa namba 7 maarufu enzi zake, David Beckham
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GRIEZMANN ASEMA KUTUA MAN UNITED NI "6 KWA 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top