• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 31, 2017

  WENGER ATHIBITISHA MAPENZI YAKE ARSENAL BAADA YA KUSAINI MKATABA MPYA

  Arsene Wenger amethibitisha mapenzi yake kwa Arsenal baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuifundisha klabu hiyo PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  MATAJI ALIYOSHINDAA WENGER ARSENAL  

  Ligi Kuu (3): 1997–98, 2001–02, 2003–04
  Kombe la FA (7): 1997–98, 2001–02, 2002–03, 2004–05, 2013–14, 2014–15, 2016–17  
  KOCHA Arsene Wenger amethibitisha mapenzi yake kwa Arsenal baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili.
  Mfaransa huyo, anayebaki katiuka klabu hiyo ya Kaskazini mwa London ambayo amekwishaitumikia kwa zaidi ya miongo miwili, amesaini mkataba wenye vipengele vizuri Uwanja wa Emirates.
  Kufuatia miezi ya kusakamwa mfululizo na makundi ya mashabiki wa Gunners kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu chini ya Wenger, babu huyo wa umri wa miaka 67 ilikubaliwa apewe mkataba mpya katika kikao cha bodi Jumatano.
  "Naipenda hii klabu na ninaangalia mbele kufanya kazi kwa matumaini na  furaha,"amesema Wenger.
  Wenger alijiunga na Arsenal mwaka 1996 akitokea Nagoya Grampus Eight ya Japan aliyoifundisha kuanzia mwaka 1995 akitokea Monaco alikofanya kazi tangu mwaka 1987 hadi 1994 baada ya kuifundisha kwa miaka mitatu Nancy, zote za Ufaransa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WENGER ATHIBITISHA MAPENZI YAKE ARSENAL BAADA YA KUSAINI MKATABA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top