• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 24, 2017

  NUSU FAINALI U-17 AFRIKA ZACHEZWA LEO GABON

  NUSU Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 zinachezwa leo katika miji ya Libreville na Port Gentil nchini Gabon.
  Uwanja wa Port Gentil, Ghana itamenyana na Niger kuanzia Saa 9:30 Alasiri kwa saa za huku na Saa 11:30 kwa Saa za Afrika Mashariki, mchezo ambao utachezeshwa na refa Mustapha Ghorbal kutoka Algeria, atakayesaidiwa na Aymen Ismail wa Tunisia na Attia Amsaad wa Libya.
  Uwanja wa l’Amitié Sino mjini Libreville, mabingwa watetezi Mali watamenyana na Guinea kuanzia Saa 9:30 Alasiri kwa saa za huku na Saa 11:30 kwa Saa za Afrika Mashariki katika mchezo ambao utachezeshwa na Davies Ogenche Omweno wa Kenya, atakayesaidiwa na Arsenio Chadreque Marengula wa Msumbiji na Souru Phatsoane wa Lesotho.
  Mali na Ghana zinapewa nafasi kubwa ya kukutana katika Fainali ya michuano hii, kutokana na matokeo yao pamoja na kiwango kizuri walichoonyesha katika hatua ya makundi.
  Pamoja na hayo wataalamu wanaamini katika wakati mwingine mambo huenda tofauti na matarajio, hivyo hata Guinea na Niger si za kupuuzwa.
  Ghana na Guinea zimetokea Kundi A ambako zilizipiku wenyeji Gabon na Cameroon kuja hatua hii, wakati Mali na Niger zimetokea Kundi B ambako zilizizidi kete Tanzania na Angola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NUSU FAINALI U-17 AFRIKA ZACHEZWA LEO GABON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top