• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 31, 2017

  KINDA WA GHANA ALIYENG'ARA GABON ATAKIWA MAN CITY

  KLABU kadhaa za Ulaya zikiwemo Manchester City, Olympique Lyon na PSG zzimetoa ofa nzuri kwa kinda wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Black Starlets, Emmanuel Toku, baada ya kufanya vizuri kwenye fainali za U-17 Afrika mwaka huu nchini Gabon.
  Kinda huyo nyota alifunga mabao mawili kwenye mashindano hayo na akawa Mchezaji Bora wa Mechi mara mbili kati ya mechi tano alizocheza kwenye mashindano hayo.
  Na kwa mujibu wa Abdul Hayye Yartey, Rais wa Cheetah FC, klabu inayommiliki mchezaji huyo, amesema Emmanuel Toku amepata ofa kutoka Manchester City, PSG na Lyon zikitaka saini yake.
  Emmanuel Toku alikuwa Mchezaji Bora wa Mechi mara mbili katika mechi tano alizocheza Gabon

  "Tumepokea ofa PSG, Lyon za Ufaransa na Manchester City, lakini hakuna uamuzi uliochukuliwa,"amesema Yartey katika mazungumzo yake na GHANASoccernet.com
  "Tutakaporejea kutoka kwenye mashindano, tutaangalia na kuona ofa ipi ni nzuri kwake [Toku]. Toku ni mwanafunzi wa shule ya Osei Kyeretwie mjin Kumasi.
  Black Starlets ilifungwa 1-0 na Mali katika fainali ya michuano hiyo mjini Libreville, Gabon wiki iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KINDA WA GHANA ALIYENG'ARA GABON ATAKIWA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top