• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 24, 2017

  NI MAN UNITED, AU AJAX KUBEBA NDOO NDOGO YA UEFA?

  FAINALI ya michuano ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya, inatarajiwa kufanyika leo usiku Uwanja wa Friends Arena mjini Solna, Sweden ikizikutanihsa Ajax ya Uholanzi na Manchester United ya England.
  Timu hizo zimekutana mara nne kwenye michuano ya Ulaya, mar azote kwenye UEFA Cup ambayo sasa inaitwa Europa League, huku kila timu ikishinda matra mbili.
  Pamoja na hayo, Manchester United iliitoa Ajax mara zote hizo, ushindi wa jumla wa 2–1 msimu wa 1976–77 Raundi ya kwanza ya Kombe la UEFA na wa 3–2 msimu wa 2011–12 kwenye hatua ya 32 Bora ya UEFA Europa League.
  Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ataibuka kifua mbele leo?

  Hii ni fainali ya pili kwa Ajax katika michuano ya Europa League tangu inaitwa UEFA Cup, wakiwa na kumbukumbu ya kushinda taji hilo mwaka 1992 katika fainali dhidi ya Torino kwa mabao ya ugenini.
  Na hii ni fainali ya kwanza kwa Manchester United kwenye michuano hiyo tangu inaitwa UEFA Cup na wakishinda wataungana na Juventus, Ajax, Bayern Munich na Chelsea kama klabu pekee zilizotwaa mataji yiote matatu ya klabu Ulaya, Ligi ya Mabingwa, Europa League na lililokuwa Kombe la Washindi Ulaya.
  Mshindi wa mechi hiyo Mechi hiyo itakayochezeshwa na refa kutoka Slovenia, Damir Skomina atakutana na bingwa wa msimu huu wa Ligi ya Mabingwa katika mechi ya Super Cup ya UEFA mwaka huu. 
  Na pia ataingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, 2017–18.  Fainali ya Ligi Mabingwa itafuatia Uwanja wa Millennium mjini Cardiff, Wales Juni 3, mwaka huu ikizikutanisha Juventus ya Italia na Real Madrid ya Hispania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI MAN UNITED, AU AJAX KUBEBA NDOO NDOGO YA UEFA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top