• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 27, 2017

  WENGER KUCHEZA PATA POTEA LEO LANGONI, KUMPANGA OSPINA

  KOCHA mfaransa, Arsene Wenger atanataka kucheza pata potea kwa kumpanga kipa wa pili, David Ospina kwenye fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea.
  Habari za kustusha ambazo Bin Zubeiry Sports - Online imezioata kutoka Daily Mail Online zinasema kipa huyo wa kimataifa wa Colombia atadaka leo Uwanja wa Wembley badala ya kipa wa kwanza, Petr Cech, aliyefanya mazoezi kawaida tu jana.
  Uamuzi huo unakuja baada ya kujulikana pia kwamba, beki Shkodran Mustafi amepoteza nafasi ya kucheza mechi ya leo. Tayari Arsenal ilikuwa inawakosa Laurent Koscielny aliyesimamishwa na Gabriel ambaye ni majeruhi.
  Arsene Wenger anatarajiwa kucheza pata potea leo kwa kumpanga David Ospina kwenye fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Cech ni kipa mzoefu, lakini inaonekana Wenger ameamua kuendelea kumuamini Ospina baada ya kumfanya ndiye kipa wake wa mashindano ya vikombe kwa msimu huu.
  Ospina amecheza mechi 13 msimu huu zikiwemo za Ligi ya Mabingwa na Kombe kla FA. Cech alidaka katika Robo Fainali na Nusu Fainali wakati Ospina alipokuwa majeruhi na alitarajiwa kuendeleea kudaka dhidi ya timu yake ya zamani leo katika mchezo muhimu kabla ya kuhamia Fenerbahce ya Uturuki kwa dau la Pauni Milioni 5.
  Licha ya kufanya mazoezi jana, Mustafi bado anaonekana ataukosa mchezo wa leo ingawa anaendelea kupata ahueni kidogo baada ya maumivu aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Sunderland Mei 16.
  Inafahamika The Gunners imekuwa ikipambana kuhakikisha Mustafi anacheza baada ya kurejea mazoezini, lakini taratibu za kitabibu zinaweza kumfanya beki huyo wa Ujerumani aw nje leo.
  Hiyo inamaanisha Per Mertesacker anatarajiwa kuanza kwa mara ya kwanza leo msimu huu. Ikumbukwe Nahodha huyo wa klabu kutoka Ujerumani amecheza dakika 37 tu msimu huu.
  Ikiwa Wenger ataendelea kutumia mabeki watatu, Mertesacker atacheza sambamba na Rob Holding na Nacho Monreal — ambaye ni beki wa kushotio. Kieran Gibbs na Alex Oxlade-Chamberlain wanapambana kuziba pengo la Monreal katika wingi beki ya kushoto.
  Wakati huo huo, Wenger amesema kuhamia Uwanja wa Emirates Stadium kimekuwa kipindi kibaya zaidi katika maisha yake.
  Arsenal iliondoka Uwanja wa Highbury kuhamia Uwanja mpya wa Emirates baada ya kujengwa msimu wa 2006-07 season na tangu hapo hawakutwaa taji lolote rasmi hadi mwaka 2014 waliposhinda Kombe la FA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WENGER KUCHEZA PATA POTEA LEO LANGONI, KUMPANGA OSPINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top