• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 30, 2017

  HAJIB AWAAMBIA SINGIDA UNITED WAACHE MANENO WAFANYE KWELI

  Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Ibrahim Hajib Migomba amewataka viongozi wa Singida United, kuachana na kupiga simu za maneno bali waweke mzigo ili asaini mkataba wa kuitumikia kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo asubuhi, Hajib amesema kwamba amekuwa akihusishwa kujiunga na wageni hao wa Ligi Kuu, walio chini ya kocha wa zamani wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm, lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa.
  Ibrahim Hajib (kushoto) akiwa na mkewe aliyefunga naye ndoa wiki iliyopita Dar es Salaam

  Hajib amesema suala la Singida kumuhitaji halina pingamizi kutokana na kupokea simu nyingi kutoka kwa viongozi na benchi la ufundi, lakini wameshindwa kukamilisha mpango huo.
  Amesema imefikia wakati amechoshwa na simu nyingi kwa sasa, bali anahitaji kuona timu hiyo ama nyingine ambayo inamuhitaji inaweka mzigo mezani ili asaini.
  "Ni kweli napokea simu nyingi kutoka Singida, sasa zinachosha kama vipi waweke dau ambalo nalihitaji mezani nimwage wino,”alisema.
  Hajib yuko huru kwa sasa baada ya kumaliza mkataba wake Simba SC na wakati kukiwa kuna taarifa za kutakiwa na timu mbalimbali zikiwemo za Misri na Afrika Kusini, vimwaga wapya wa fedha nyingi za usajili nchini, Singida United nao wanajitokeza kutaka huduma za fundi huyo wa mpira.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HAJIB AWAAMBIA SINGIDA UNITED WAACHE MANENO WAFANYE KWELI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top