• HABARI MPYA

  Sunday, May 28, 2017

  NDIKUMANA YUKO TAYARI KUUNGANA NA MAVUGO SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  KIUNGO wa ulinzi wa kimataifa wa Burundi, Youssouf Ndikumana amesema kwamba yuko tayari kujiunga na washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba SC iwapo watafika bei yake.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana mjini Dodoma, mchezaji huyo wa Mbao FC ya Mwanza alisema kwamba kwake anaangalia maslahi na kama Simba wataweza kutoa kiwango cha fedha anachotaka atajiunga nao.
  Youssouf Ndikumana (kulia) katika mahojiano na mwandishi wa habari, Saada Akida jana mjini Dodoma 

  "Mimi nipo tayari kujiunga Simba au timu yoyote kati ya hizo zinazotajwa zinanitaka, kikubwa ninaangalia maslahi," alisema.
  Ndikumana alicheza vizuri jana katika fainali ya ASFC, ingawa Mbao FC ililala 2-1 mbele ya Simba SC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
  Na wakati tayari kuna tetesi za mchezaji huyo kutakiwa na Simba SC, naye amesema yuko tayari kwenda kuungana na Mrundi mwenzake, mshambuliaji Laudit Mavugo.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDIKUMANA YUKO TAYARI KUUNGANA NA MAVUGO SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top