• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 29, 2017

  TFF YAZIITA KLABU LIGI KUU, DARAJA LA KWANZA KWA MAREKEBISHO YA KANUNI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezitaka klabu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/18 kuwasilisha maoni na mapendekezo mbalimbali kuhusu marekebisho ya kanuni za ligi hiyo.
  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema leo kwamba, zoezi hilo litafanyika kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) msimu wa 2017/18.
  "TFF inaagiza klabu zote - kwa nafasi walizonazo kama wanafamilia ya mpira wa miguu, kuwasilisha mapendekezo na maoni kuhusu marekebisho ya katiba kwa njia ya kuyatuma kupitia anwani za sanduku la Barua 1574, Dar es Salaam au barua pepe tplb.tplb@yahoo.com au yaletwe moja kwa moja ofisi za Bodi ya Ligi au TFF,"amesema Lucas.
  Lucas amesema maoni hayo yatafanyiwa kazi na Bodi ya Ligi kabla ya kupelekwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ambacho ndiyo kitayapitisha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAZIITA KLABU LIGI KUU, DARAJA LA KWANZA KWA MAREKEBISHO YA KANUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top